Mapishi ya nundu
Kuandaa: dakika 30
Mapishi: dakika 15
Mapishi: dakika 15
Walaji: 3
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Mahitaji
- Nyama lakini iwe nundu
- Tangawizi ya unga
- Vitunguu saumu
- mdalasini
- Chumvi
- Soy sauce
- Currypowder
- Pilipilimanga
- Maji
- Vitunguu maji visage viwe uji
- Ndimu
Maelekezo
- Osha nyama vizuri, ikamulie ndimu ya kutosha. Weka tangawizi kiasi na vitunguu saumu kisha bandika jikoni.
- Hakikisha nyama imeiva vizuri sana, ibaki na mchuzi kidogo.
- Weka vitunguu maji ulivyovisaga kisha funika. Iache iendelee kuchemka vitunguu viive.
- Hakikisha mpaka maji yanakauka, hiyo nyama inamafuta sana.
- Itaanza kujikaanga hapo weka mdalasini na curry powder koroga mpaka uone nyama inabadilika rangi kua ya kahawia, usiache kukoroga mana itashika chini.
- Ongeza soy sauce au oyster sauce au sause yoyote uliyonayo. Koroga ichanganyikane vizuri na nyama yako.
- Ongeza tangawizi na pilipili manga, unaweza kutumia hata pilipili mbuzi.
- Koroga mpaka yale maji ya soy sauce yakauke, kamulia ndimu koroga kwa dakika 5 msosi wako utakua tayari.
Mishkaki Ya Kuku -1
MahitajiKuku kidari (boneless breast) 4 Ratili (LB)Mafuta ya kukaangia kiasiVitunguu 3Nyanya 3Pilipili boga 2Masala Ya Kuloweka Katika Kuku:Kitunguu saumu/thomu na tangawizi iliyosagwa 1 kijiko cha supuPilipili mbichi iliyosagwa 1 kijiko cha supuMtindi 2 vijiko vya supuNdimu 3 vijiko vya supuChumvi kiasiJiyrah (cummin powder/bizari ya pilau) 1 kijiko cha supuDania (coriander powder/gilgilani) 1 kijiko cha chaiPilipili nyekundu ya unga 1 kijiko cha supuMdalasini wa unga 1 kijiko cha chaiAu tumia ukipenda bizari za mishkaki za tayari kama tanduri masala.Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
1. Kata kuku vipande vikubwa kubwa kiasi .2. Changanya kuku na masala ya vitu vyote katika masala ya kurowekea kuku uroweke kwa muda wa masaa.3. Katakata vitunguu, nyanya, pilipili boga vipande kiasi.4. Tunga vipande vya kuku katika vijiti vya kuchomea kababu (kabaab skewers) huku unatunga baina yake kitunguu, nyanya, pilipili boga.5. Tia mafuta kiasi katika kikaango. Mafuta yasiwe mengi hadi yakafunika kuku.6. Tumia mafuta kidogo kidogo kila unapoepua kabaab za kwanza ikiwa yamekauka, unaongeza mafuta kidogo kama kiasi ya robo kikombe.7. Kaanga kababu za kuku katika moto wa kiasi ukiwa unazigeuza geuza hadi kuku awive.8. Epua, weka katika sahani ikiwa tayari kuliwaMISHKAKI YA NG’OMBE NA PAKO LA GILIGILIANI
Watu wengi wamezoea kula mishkaki nje ya nyumbani na niwachache sana wanaotengeneza mishkaki nyumbani.
Tofauti na mishkaki unayokula mtaani na kwenye migahawa,mishkaki ya nyumbani unaweza kuiandaa na kuichoma katika ubora zaidi na ukaipa vionjo vinavyovutia ambavyo mara nyingi huwezi kuvipata kwenye mishkaki unayokula nje ya nyumbani.
Mahitaji
1.Nyama
- Nyama ya Ng’ombe kili moja (steki)
- Vitunguu swaumu vijiko 2 vya chakula
- Tangawizi vijiko 2 vya chakula
- Giligiliani ya mbegu vijiko 2 vya chai(saga iwe unga)
- Vinega au limao Vijiko 5 vya chakula
- Binzari manjano kijiko 1 cha chakula
- Chumvi kwa ladha upendayo
- Mafuta ya maji nusu kikombe
- Giligiliani ya majani vijiko 3 vya chakula(ponda iwe laini kama uji)
- Mustard ya Njano (Nashauri ya American garden)
- Hoho.
- Katoti
- Vitunguu
- Nanasi
- Kata umbo upendalo
1.Changanya vizuri mahitaji yote ya namba moja.Funga kwenye mfuko wa plastiki au bakuli la plastiki lenye ufuniko.Weka frijini kwa masaa 3 adi 5
2.Toa nyama frijini kisha chomeka kwenye miti ya mishkaki.weka mapambo pia(mboga za majani).chomeka Nyama nyingi upendavyo.nashauri Tano kwa kila mti
3.Changanya mahitaji yote ya namba 2 kwenye bakuli ili kupata pako
4.Kwa kutumia brashi ya jikoni.pakaa pako kwenye Mishkaki yote.
5.pakaa mafuta waya au wavu wa kuchomea nyama.kisha panga mishkaji na uchome kwenye moto mdogo.pakaa pako kila unapogeuza au kila mara
5.Choma kwa dakika 5 adi 8 kila upande .Tayari kwa kula.
Maelezo ya ziada.

- Unapochoma usiache ikakauka sana,mishkaki mikavu haipendezi na nimigumu kutafuna
- Pako kazi yake nikuipa nyama ladha nzuri na kuipa unyevu ili isikauke na kua kavu
Roast ya nyama iliyoungwa na karanga
Kuandaa: dakika 15 Mapishi: dakika 30Walaji: 4Ujuzi: WastaniGharama: NafuuMahitaji
- Nyama - 1/2 kilo
- Karanga zilizosagwa/ peanut butter - vijiko 3 vikubwa
- Mafuta ya kula - 1/4 lita
- Chumvi
- Tangawizi - 1
- Kitunguu saumu - 1
- Kitunguu maji - 2
- Nyanya - 4
- Nyanya chungu - 4
- Cube magic
- Viazi - 6
- Viungo vingine upendavyo kwenye sauce*.
Maelekezo
- Tayarisha nyama - kata, osha, weka chumvi, tangawizi na kitunguu saumu. Acha ikae kwa dakika 45 hadi saa 1 ili viungo viingie vizuri.
- Bandika sufuria jikoni, weka mafuta kiasi. Subiria yapate moto.
- Weka nyama kwenye mafuta. Fanya kama unaikaanga - koroga ili ichanganyike vizuri na mafuta. Funika sufuria au chungu na mfuniko ili nyama ijipike kwa mvuke wake vizuri.
- Geuza geuza nyama kila mara ili kuzuia isigande kwenye chombo cha kupikia. Subiria hadi iive.
- Unaweza kubadilisha sufuria maana utakayokaangia nyama itakuwa na mafuta yenye masalia ya viungo. Badilisha sufuria kwa kumimina mafuta kwenye sufuria nyingine, acha ipate moto - weka mafuta na kisha weka nyama yako ili uendelee na mapishi.
- Weka vitunguu kwenye nyama, koroga hadi viive.
- Weka nyanya, koroga kisha funika. Subirie zipate kuiva.
- Ongeza karoti, pilipili hoho, na viambato vingine utakavyo.
- Anza kuandaa peanut butter (au karanga za kusaga) kwa kuweka vijiko 3 ya vikubwa kwenye bakuli ya plastiki.
- Ongeza maji ya uvuguvugu kiasi, na uanze kusaga, kukoroga au kufinyanga kwa mkono ili karanga zichanganyike vizuri na maji kuwa kama uji mzito. Ni vizuri ukipata rojorojo nzuri maana itakuwa rahisi kuchanganyika na mchuzi.
- Ukishapata mchanganyio mzuri, weka karanga kwenye chungu cha nyama jikoni. Koroga hadi mchanganyiko uwe vizuri. Ongeza maji kama robo kikombe ili upate kulainisha rojo. Funika chungu chako.
- Menya, osha na kata viazi mviringo vyako kwenye vipande vidogo na hifadhi kwenye maji.
- Menya osha na kata nyanya chungu - au unaweza kuweka zikiwa nzima nzima.
- Mchanganyiko ukishachemka, Weka viazi na nyanya chungu. Subiria mchanganyiko uchemke, halafu weka cube maggi. Koroga ili kuifanya ichanganyike vizuri na mboga.
- Unaweza kuongeza tui la nazi au maziwa kuongeza ladha ya mboga.
- Subiria dakika 4 hadi 5 baada ya kuongeza cube maggie kisha ongeza pilipili manga ya kusaga. Weka pilipili manga mwisho sababu ikiwa hupoteza ladha kirahisi kwenye moto mkali.
- Viazi vikishaiva, unaweza kutenga mboga yako na chakula ujirambe.
njema sana
JibuFutambarikiwe
Good
JibuFuta