Alhamisi, 12 Machi 2015

Kashata

Kashata Za Njugu-Karanga

Vipimo:

Karanga                                             Kilo
Sukari                                                5 vikombe
Maji                                                    2 vikombe
Maziwa ya unga                                  2 vijiko vya chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
    
1.                  Saga karanga zilizokaangwa na kumenywa mpaka zilainike kiasi.
2.                  Kisha changanya maji na sukari weka jikoni yachemke mpaka yanate kidogo kama shira. Changanya unga wa karanga na maziwa ya unga kisha mimina kwenye hiyo shira.
3.                  Koroga taratibu kwa moto mdogo mpaka uone imeshikana na inanata.
4.                  Paka mafuta treya  kisha mimina na utandaze upesi upesi.
5.                  Acha ipoe kidogo tu kisha katakata vipande na acha ipoe kabisa.
6.                  Panga kwenye sahani tayari kwa kuliwa pamoja na kahawa.

Kidokezo:
Kama maziwa ya unga huna si lazima

Kashata za njugu


Mahitaji

Karanga Sukari Unga wa iliki . Maji
Namna ya kutengeneza Kaanga karanga, kisha zitoe maganda yote ziwe nyeupe. peta ili kuyatoa magamba kirahisi. Chukua sukari uchanganye na maji kidogo upike mpaka iwe nzito
Changanya unga wa iliki, kisha chukua karanga zako mimina katika sukari iliyoyeyushwa
Koroga koroga kwa mwiko mpaka ile sukari uliyoikausha ikauke Kisha mimina haraka katika sinia iliyopakwa samli kidogo na utandaze
Baadae chukua kisu ukate kate kashata zako. Zikishapoa kashata zako zitakuwa tayari kwa kuliwa

 

Kashata za nazi

Mahitaji

  • Sukari kikombe 1
  • Nazi kikombe 1
  • Mdalasini wa kusaga nusu kijiko cha chai
  • Cardamon nusu kijiko cha chai
  • Maziwa vijiko 2 vya chakula
  • Unga wa ngano (option)
  • Rangi ( option)

Maelekezo

  • Pasua nazi, toa ile nyama ya ndani weka kwenye blender, weka na maziwa saga mpaka iwe laini sana. Au unaweza kukuna kwa kutumia kibao cha mbuzi.
  • Washa moto, bandika sufuria jikoni likipata moto weka sukari, koroga mara kwa mara mpaka iyeyuke na kua brown.
  • Punguza moto, weka nazi, mdalasini, cardamon, rangi, unga koroga vizuri kwa dakika 2 ili mchanganyiko uchanganyikane.
  • Chukua sinia lipake mafuta, toa mchanganyiko ule jikoni umwage kwenye sinia chukua kijiko, usambaze uenee vizuri.
  • Uache upoe kwa muda.
  • Kata saizi unayotaka ukiwa bado wa moto, ukimaliza uache upoe kisha jirambe kwa nafasi

Maoni 1 :

  1. asante sana kwa hii recipe nimefurahi sana kupatilia hapa

    JibuFuta