
usafishaji wa friji kwa kutumia magadi soda, hapa nitaelezea jinsi ya kufanya hivyo
Mahitaji
- Magadi soda
- Beseni dogo
- Kitambaa laini
- Sponge
1. Zima friji yako na kisha toa vitu vyote vilivyomo ndani.
2. Weka maji kwenye beseni dogo na kisha changanya na vijiko viwili vya magadi soda.
3. Chukua sponge na uanze kufuta friji yako kuanzia juu kabisa hadi mwisho, safisha vizuri kila mahali na kwa ufasaha kuhakikisha kila uchafu umetoka. Toa containers zote na uzisafishe kwa pembeni na kuzisuuza kisha urudishie mahali pake.
4. Chukua maji masafi na kitambaa laini kisha ufute jokofu lako kama kusuuza vile.
5. Baada ya muda panga vitu vyako vizuri na washa jokofu lako.
Magadi soda husaidia kung’arisha na kuondoa harufu ambayo sio nzuri
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni