Jumapili, 8 Machi 2015

JUISI YA MCHANGANYIKO WA MATUNDA




MAHITAJI
450 grams Nanasi
 50 grams Tangawizi fresh osha vizuri menya
1 Carrot, 
 
JINSI YA KUANDAA FUATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPO CHINI
Muda wa maandalizi : Dakika 15 
Muda wa mapishi : Dakika 15
Idadi ya wanywaji : watu wawili
Tunda la nanasi na karoti vinachangia sana sukari yote ambayo juisi inatakiwa iwenayo. Tangawizi inaweka uwiano sawa wa ladha kati ya nanasi na karoti, kama sio mpenzi wa tangawizi sio lazima kuitumia, lakini kama ni mpenzi wa nanasi au karoti unaweza kuzidisha  kimojawapo ili upate ladha halisi ya unachokipenda.
Tangawizi: Inategemea na ubora wa tangawizi, unaweza kuhitaji nyingi zaidi au wastani cha msingi uweze kupata harufu mwanana katika juisi yako.


Menya vizuri nanasi yako kisha katakata vipande vidogo kama inavyoonekana 


Chukua vipande vya nanasi, karoti na tangawizi kisha saga kwenye blenda.


Saga vizuri kisha chuja vizuri kwa chujio iliyo safi.


Baada ya kuchuja kama haijachujika vizuri, basi ongeza maji baridi na safi kiasi tu kisha chuja tena na kisha utapata juisi safi kabisa laini


Kwa sasa ipo tayari waweza kumpatia mnywaji ikiwa ya baridi. Kinywaji safi kabisa kwa majira ya joto yanayokuja hivi karibuni. Waandalie familia yako waweze kufurahia na nakuwajengea tabia ya kuzoea kunywa maji.

AINA MBALIMBALI ZA JUISI NA KAZI ZAKE MWILINIZipo juisi za namna tofauti na matumizi yake yanategemea na malengo ya mtumiaji. Nadhani watumiaji wengi wanakunywa juisi bila kujua umuhimu au kazi yake mwilini. Wengi hawajui ni juisi gani itumike wakati gani.

Hebu fuatilia aina zifuatazo na upate kujua utengenezaji wake na kazi zake.

  • JUISI YA KAROTI NA APPLE: Chukua kiasi cha karoti na apple kinachotosha kutengeneza juisi kwa kiasi ulichokusudia. Usikose kipande cha limao kiasi cha nusu. Anza kuandaa juisi yako kwa kuosha na kumenya karoti na apple kisha katakata katika vipande vidogo vinavyoweza kusagika kirahisi kwenye blenda. Saga mchanganyiko wako ili upate juisi. Baada ya kupata mchanganyiko wa juisi yako kamulia limao kwa ajili ya kuongeza ladha. Unaweza kuiweka kwenye friji ili ipate ubaridi kidogo na tayari kwa kuinywa. Siyo lazima kuongeza sukari kwenye juisi kwani matunda yana sukari asilia.
  • JUISI YA KAROTI NA APPLE ina uwezo wa kutunza ngozi kwani tunda la apple linaondoa uchafu kwenye ngozi na karoti nayo kwa kutumia kirutubisho cha beta-karotini chenye uwezo wa kutengeneza Vitamin A hulinda na kurejesha uhai katika ngozi ambapo inaifanya ionekane nyororo. Pia juisi hii husafisha tumbo na kuondoa uchafu tumboni. Aidha juisi hii inafanya ini lifanye kazi yake vizuri kwa kulainisha nyongo na kusaidia kuondoa uchafu.

  • JUISI YA VIAZI MVIRINGO: Chukua viazi mviringo vinavyotosha kwa juisi. Andaa kwa kuviosha na kumenya kisha katakata vipande vidogo kwa ajili ya kuvisaga. Saga ili upate juisi uliyoikusudia.
  • JUISI YA VIAZI MVIRINGO inatumika kama dawa ya kuondoa au kupunguza asidi au gesi tumboni. Juisi ya viazi mviringo inaweza kusaidia kupunguza matatizo ya figo, kisukari, unene au kitambi.

  • JUISI YA MBOGAMBOGA: Juisi hii ina mchanganyiko wa mbogamboga kam vile karoti, nyanya na matango. Maandalizi yake ni kam juisi nyingine. Anza kwa kuosha kisha kumenya na kukatakata vipande. Saga mchanganyiko huo kwenye blenda ili upate juisi uliyoikusudia. Unaweza kuweka kwenye friji ili ipate ubaridi kidogo.
  • JUISI hii inasadaidia kuzuia kansa hasa ile ya kwenye mfumo wa kumeng`enya chakula, kukinga mapafu na artery. Pia inasaidia kuimarisha kinga.

  • JUISI YA TIKITI MAJI: Chukua tikiti maji (watermelon) na osha kisha likate vipande na chukua nyama yake ya ndani ambayo utaisaga na kupata juisi.
  • JUISI YA TIKITI MAJI ina uwezo wa kusafisha figo pamoja na njia ya mkojo. Inazuia unene kwa kuwa na kiwango kidogo cha calories.
KWA aina hizo chache za juisi unaweza kujua umuhimu wa juisi za matunda na mbogamboga tunazotumia. Kwa leo ninaishia hapo na siku zijazo nitaendelea kukupatia ufahamu kwa aina zingine za juisi pamoja na kazi zake.
SIKU NJEMA.

JUISI YA AVOCADO AU PARACHICHI





JUISI HII YA PARACHICHI INA VIRUTUBISHO VINGI SANA KATIKA MWILI NI TIBA KWA AFYA YA MLAJI TENGENA KWAJILI YA FYA YA FAMILIA YAKO




Kata parachichi nusu kama inavyoonekana katika picha



Kisha toambegu ya kati kati chukua kijiko toa nyama ya ndani weka katika blenda kwajili ya kusaga pamoja na matunda mengine

Mahitaji

1 parachichi lililoiva
2  ndimu safi zenye maji ya kutosha
50 gram maji safi ya baridi
2 vipande viwili vya papai la kuiva
3 sukari kijiko kikubwa cha chakula
2 asali kijiko kikubwa ca chakula
5 gram chumvi

Kwa ladhazaidi unaweza ngezea jani la fresh mint sio lazima 

Jinsi ya kuandaa:

WEka katika blenda parachichi, vipande vya papai, jani la mint kisha anza kusaga wakati unasaga unaongezea maji kiasi ili mchanganyiko usiwe mzito sana ukashindwa kuchanganyika . Mwisho kabisa ongezea asali, chumvi, limao na sukari kisha blend vizuri upate mchanganikio safi na wenye ladha safi.

Kisha weka katika friji ipoe nakushauri juisi hii kunywa muda wa mchana wakati huu mwili unakua umejiandaa kupekea virutubisho vilivyopotea. Safi sana kwa mtu mzima na mtoto pia ni nzuri sana kwa wale wanaozingatia mlo safi ili wasiongezeke uzito.  


IPATIE GLASI MOJA ANGALAU KILA BAADA YA SIKU 2 JUISI HII INA LADHAYA KIPEKEE

Maji ni muhimu sana kwa afya yako, ukinywa maji kwa siku katika kiwango kinachotakiwa kiafya utaondokana na matatizo mengi ambayo mengine ungelazimika kutumia dawa mfano vidonge vya kupunguza maumivu (pain killers) na matatizo mengine yanayohusiana na uchovu wa mwili. 

Kabla sijaorodhesha faida mbalimbali ni vizuri ujue, je kama ukipungukiwa na maji mwilini ni athari au mataizo gani unayopata? Ukipungukiwa na maji mwilini unaweza kujisikia uchovu, kichwa kuuma, ngozi kukakamaa kutokana na kukauka, chakula kutosagwa vizuri ambapo unaweza pata shida kujisaidia haja kubwa nakadhalika.


Vilevile kama ukipungukiwa na maji mwilini utaweza kuwa na hizi dalili,

  • Kuhisi kiu au wakati mwingine hata kwikwi.
  • Kuhisi njaa. (Watu wengi hudhani kuhisi njaa ni dalili ya kutakiwa kula chakula, lakini ukweli ni kwamba wakati mwingine kuhisi njaa ni dalili ya kutakiwa kunywa maji.)

Je unatakiwa kunywa maji kiasi gani kwa siku? Wataalamu wa afya wanashauri unywe maji angalau glasi 8 (ikiwa glasi 1 ina ujazo wa 250ml) sawa na lita 2 kwa siku.


Baada ya kujua dalili za ukosefu wa maji mwilini pamoja na matatizo utakayopata kama hutokunywa maji ya kutosha kulingana na mahitaji ya mwili. 


Hizi ni tabia nzuri za kiafya za kuzizingatia.
  • Kila uamkapo asubuhi kunywa angalau glasi moja (1) ya maji.
  • Kila unapotaka kula, kunywa maji kabla ya kuanza kula chakula chako. Vilevile kunywa maji wakati ukiendelea kula na mwisho wa kula chakula kunywa maji tena.
  • Kabla ya kuanza kufanya mazoezi pendelea kunywa maji kwanza. Kunywa maji glasi 1 au 2 dakika 30 kabla ya kuanza kufanya mazoezi.
Kwakuwa maji ni muhimu na yana kazi nyingi mwilini, zifuatazo ni faida za maji mwilini kiafya.

1. Maji huboresha ngozi.


Seli za ngozi zinahitaji maji kwaajili ya utendaji kazi mzuri wa kazi zake ikiwemo kulinda ngozi kwa kupambana na magonjwa mbalimbali yakiwemo eczema, psoriasis na hata makunyanzi na kukauka kwa ngozi. Hivyo ukitaka kuonekana mwenye ngozi nzuri kama ya mtoto penda kunywa maji kwa kiwango kinachotosha kila siku kuboresha afya ya ngozi yako.

2. Maji husaidia katika utendaji kazi wa ubongo.


Ukitaka kuwa mwenye akili safi na mwepesi wa kufikiri na kutatua mambo mbalimbali yanayohitaji kutumia akili, pendelea kunywa maji pamoja na vyakula vyenye kusaidia seli za ubongo kufanya kazi zake vizuri. Ubongo unahitaji maji, hewa safi ya oxygen na vyakula vyenye virutubisho kama njugu mawe, mafuta ya samaki (fish oil), nyanya na mbegu za maboga. 


Kujua zaidi: Soma Namna ya kutunza afya ya akili na mwili wako


3. Maji husaidia usagaji wa chakula.


Mfumo wa umeng'enyaji wa chakula (digestive system) hutegemea sana maji katika ulainishaji wa chakula na hivyo kuwezesha virutubisho vya chakula kutumika vizuri na mwili, kwakuwa maji hulainisha chakula, pia huepusha kupata choo kigumu (constipation).

4. Maji husaidia kuondosha sumu na taka mwilini.


Licha ya maji kuwa ni sehemu kubwa ya miili yetu pia ni kitu ambacho kinawezesha viungo vingine muhimu kama moyo katika usukumaji damu yenye kiwango kikubwa cha oxygen ambayo inabeba maligafi nyingi na kupeleka sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo katika ini na kwenye figo ambapo uchujaji wa taka mwilini hufanyika.

5. Maji husaidia kupunguza maumivu mbalimbali kama ya kichwa pamoja na mgongo.


Licha ya kuwa na sababu nyingi za mtu kupata maumivu ya kichwa lakini pia ukosefu wa maji mwilini ni sababu moja wapo ya kichwa kugonga kwasababu ya kupungukiwa na mahitaji muhimu kama oxygen ambayo husafirishwa na damu ambapo maji husaidia kurahisisha shughuli hizo.

6. Maji huusaidia mwili kupigana na magonjwa mengi kama ya mafua, tumbo, saratani za aina mbalimbali na matatizo mengine ya figo.


Maji pamoja na juisi ya malimao husaidia sana kupooza magonjwa kama ya kikohozi, mafua, kuchafuka kwa tumbo, satani ya tumbo na kibofu cha mkojo nakadhalika. Maji yanaweza kukuepusha au kupunguza makali ya magonjwa hayo kwa kusaidia mwili wako kuongeza kinga ya mwili.

7. Maji husaidia kupunguza uzito.


Kama nilivyosema hapo awali wakati mwingine unaweza hisi kuwa unahitaji kula kumbe unahitaji kunywa maji kwakuwa umepungukiwa na maji mwilini. Ni mara ngapi umekuwa ukitamani kula chakula kwa pupa lakini baada ya kunywa maji ukajikuta unakula kidogo kuliko ulivyotegemea hapo awali. 

Uzito wa mwili hutegemea sana ulaji wa chakula pasipo kufanya mazoezi, maji pia husaidia kuondoa taka za vyakula vya mafuta (fats by-products) na kukuwezesha uwe mwenye afya bora.

Unaweza soma pia: Njia 5 za kupunguza uzito wa mwili

8. Maji husaidia kuboresha misuli na kulainisha jointi za viungo vya mwili.


Maji ni chanzo cha nguvu mwilini, misuli huifadhi nguvu ya ziada itakayotumika iwapo nguvu ya mwili itapungua. Kunywa maji kulingana na mahitaji ya mwili wako ili kuwezesha utumikaji mzuri wa chakula na uhifadhi wa uhakika wa nguvu mwilini. Maji pia yatakusaidia kulainisha viungo vyako vya mwili kama jointi za kwenye magoti, vidole vya mikono na miguu n.k.

Maoni 5 :

  1. safi kabisa
    tunashukuru kwa elimu hii nzuri na muendelee kutuhabarisha zaidi

    JibuFuta
  2. safi kabisa
    tunashukuru kwa elimu hii nzuri na muendelee kutuhabarisha zaidi

    JibuFuta
  3. Elimu nzuri somo limeeleweka kabisa

    JibuFuta