Ijumaa, 13 Februari 2015

Roast ya Nyama ya Nguruwe(Kitimoto)


Nyama ya nguruwe ni nyama laini na yenye ladha nzuri inapopikwa vizuri, nyama hii. Leo nawaletea mapishi ya rosti.
Mahitaji
  • 1/2kg Nyama ya nguruwe 1/2 kilo
  • Nyanya6  zilizoiva 6
  • Karoti 2
  • Pilipili hoho 1
  • Ndimu 1
  • Chumvi
  • 2Tbsp Mafuta 
  • Vitunguu saumu 2
Matayarisho
1. Safisha nyama kisha kata kata vipande vidogo kiasi kulingana na unavyopendelea na kisha weka kwenye chombo kikavu
2.  Menya vitunguu saumu na vitwange.
3. Changanya nyama yako na vitunguu saumu, kamulia ndimu na weka chumvi kiasi cha kutosha.
4. Bandika kikaango chako jikoni kisha weka mafuta kiasi kama nyama yako haina mafuta ya kutosha na yakianza kuchemka weka nyama yako.
5. Ukiwa unasubiria nyama ikauke na kuwa ya kahawia ( kumbuka kuigeuza geuza lakini usiifunikie),  kwangua nyanya zako na karoti kwa kutumia grater au blender (kwangua nyanya tofauti na karoti) na kata kata pilipili hoho katika vipande vidogo vidogo.
6. Nyama ikiwa imeshabadilika rangi na kulainika vizuri weka karoti yako uliyoikwangua na koroga ichanganyike vizuri na nyama, acha iive kwa muda mfupi kisha weka na hoho zako. Vikilainika weka nyanya yako uliyoisaga na kukoroga vizuri kisha acha ichemke bila kuifunikia huku ukiwa unaigeuza geuza.
7. Ikiwa tayari epua na iandae ikiwa bado moto. Inaweza kuliwa kwa ugali, ndizi za kukaanga, viazi vya kikaanga, viazi vya kusaga n.k

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni