Ijumaa, 13 Februari 2015

Kababu (Meat Ball)

meatballsmeatballs      . Leo tuangalie mapishi ya meat ball(kababu) za nyama ya ng’ombe. Ni kitafunwa kizuri sana kwa asubuhi au hata jioni.
Mahitaji
  • Nyama ya kusaga 1/2kg
  • Yai 1
  • Kitunguu maji 1
  • Kitunguu saumu kilichosagwa kijiko 1
  • Pilipili manga kijiko cha chai
  • Chenga za mkata (bread crumbs)  kikombe cha chai
  • Kotmir majani 3
  • Chumvi kiasi
  • Mafuta ya kupikia
Matayarisho
1. Katakata vitunguu maji vipande vidogo vidogo, kisha changanya nyama ya kusaga, vitunguu maji ,kotmiri iliyokatwakatwa, vitunguu saum (tangawizi ukipenda), na chenga za mkate.(Ukitumia chenga za mkate halisi ni nzuri zaidi kuliko zile spesho za madukani). Weka chumvi na pilipili manga. Waweza pia weka pilipili mbuzi kama utapendelea.
2. Pigapiga yai na kisha uchanganye kwenye mchanganyiko wako, hakikisha vimechanganyika kabisa. Kisha tengeneza madoge madogo ya mviringo na weka pembeni. Hakikisha madonge sio makubwa sana ili nyama iweze iva vizuri.
3. Weka kikaango jikoni na mafuta na kiasi ili madonge yako yasizame, weka kababu zako kwenye mafuta na ziache ziive upande mmoja kisha geuza na upande mwingine. Zingatia moto uwe wa kiasi ili zisibabuke bali ziive hadi ndani kabisa.
4. Epua na weka kwenye sinia yenye karatasi za jikoni ili zichuje mafuta yote kisha weka mezani tayari kwa kula.
Waweza kula na chai, juis, soda au hata mchuzi wa maharage, mboga za majani n.k jinsi upendavyo mwenyewe

Mchemsho wa Samaki



  Tunaangalia mapishi ya mchemsho wa samaki. Mchemsho huu ni kwa ajili ya watu wawili.

Mahitaji
. Samaki wakubwa kiasi 2  . Viazi mviringo 5

. Bamia, karoti, pilipili hoho na kitunguu maji
. Tangawizi
. Ndimu 2
. Chumvi


Matayarisho
1. Andaa samaki na kisha ukamulie ndimu moja.
2. Menya viazi na ukate vipande vinne kila kiazi.
3. Katakata bamia, karoti, kitunguu na pilipilh hoho.
4. Menya tangawizi na uitwange.
5. Bandika viazi na maji kiasi kisha weka chumvi na vitunguu.
6. Vikianza kuiva weka tangawizi, hoho, karoti, bamia na samaki. Hakikisha kuna supu ya kutosha ila isiwe nyingi sana.
7. Acha vichemke kwa dakika kumi hadi 15 kisha epua.

Andaa mezani ukiweka kipande cha ndimu, nyanya na tango.

Roast ya Nyama ya Nguruwe(Kitimoto)


Nyama ya nguruwe ni nyama laini na yenye ladha nzuri inapopikwa vizuri, nyama hii. Leo nawaletea mapishi ya rosti.
Mahitaji
  • 1/2kg Nyama ya nguruwe 1/2 kilo
  • Nyanya6  zilizoiva 6
  • Karoti 2
  • Pilipili hoho 1
  • Ndimu 1
  • Chumvi
  • 2Tbsp Mafuta 
  • Vitunguu saumu 2
Matayarisho
1. Safisha nyama kisha kata kata vipande vidogo kiasi kulingana na unavyopendelea na kisha weka kwenye chombo kikavu
2.  Menya vitunguu saumu na vitwange.
3. Changanya nyama yako na vitunguu saumu, kamulia ndimu na weka chumvi kiasi cha kutosha.
4. Bandika kikaango chako jikoni kisha weka mafuta kiasi kama nyama yako haina mafuta ya kutosha na yakianza kuchemka weka nyama yako.
5. Ukiwa unasubiria nyama ikauke na kuwa ya kahawia ( kumbuka kuigeuza geuza lakini usiifunikie),  kwangua nyanya zako na karoti kwa kutumia grater au blender (kwangua nyanya tofauti na karoti) na kata kata pilipili hoho katika vipande vidogo vidogo.
6. Nyama ikiwa imeshabadilika rangi na kulainika vizuri weka karoti yako uliyoikwangua na koroga ichanganyike vizuri na nyama, acha iive kwa muda mfupi kisha weka na hoho zako. Vikilainika weka nyanya yako uliyoisaga na kukoroga vizuri kisha acha ichemke bila kuifunikia huku ukiwa unaigeuza geuza.
7. Ikiwa tayari epua na iandae ikiwa bado moto. Inaweza kuliwa kwa ugali, ndizi za kukaanga, viazi vya kikaanga, viazi vya kusaga n.k